MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AKAZA MWENDO KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA WILAYA YAKE
Na.Issack Gerald Bathromeo-Tanganyika Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh.Saleh Muhando ameahidi kulishughulikia swala la mgogoro wa ardhi katika eneo la Lyamgoroka eneo ambalo linaonekana kuwa limeuzwa na mwenyekiti wa kijiji hicho kinyume cha sheria ya ardhi.