VIJANA WATII AGIZO LA MKURUGENZI WA MANISPAA KUTOSAFISHA VYOMBO VYA USAFIRI KATIKA VYANZO VYA MAJI
Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda
Vijana na watu waliokuwa wakitumia
mto Mpanda eneo la daraja linalotenganisha Kata ya Mpanda Hotel na Misunkumilo
kusafisha magari na vyombo vingine vya usafiri,wamesitisha shughuli hiyo kutii
agizo la mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda akiwataka kutofanya shughul hiyo kwa
lengo la kulinda vyanzo vya maji.
Baadhi ya vijana waliokuwa
wakitegemea shughuli hiyo ya kusafisha magari,wakizungumza na Mpanda Radio,wamekiri
kuondoka eneo hilo ambapo hata hivyo wamesema kuondoka kwao eneo hilo kunawaahtiri kiuchumi kwa kuwa hawana vyanzo
vingine vya mapato kuendesha familia zao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa
Misunkumilo Bw. Katabi Jonas,pamoja na mambo mengine ameiomba serikali ya
Manispaa ya Mpanda kwa kushirkiana na serika;li ya Mtaa kuwasaidia vijana
kutengeneza miradi ya maendeleo kwa kuwa kila eneo wanalofanya shughuli
wanaondolewa kwa madai kuwa ni uvamizi wa maeneo.
Amesema kuwa watu zaidi ya 70
waliokuwa wakijipatia kipato kutokana na
shughuli ya kusafisha magari,pikipiki na vyombo vingine vya usafiri ambao wamepigwa
marufuku,wengi wao ni vijana waliofukuzwa eneo la uchimbaji wa kokoto milima wa
Kampuni kwa madai kuwa eneo linalochimbwa ni miliki ya Jeshi la Wananchi
Tanzania(JWTZ)
Kwa mjibu wa Mwenyekiti wa mtaa wa
Misunkumilo ambaye eneo eneo hilo lipo katika eneo lake,amesema kuwa katazo la
kusafisha magari limekuwa likitolewa mara kwa mara amba-po mpaka sasa ni takribani miaka 25.
Agizo la mwisho la Mkurugenzi
kuwataka watu kutotumia mto Mpanda kusafisha magari na vyombo vingine vya usafiri lilitolewa Ijumaa
ya wiki iliyopita.
Hivi karibuni,miongoni mwa wakazi ambao
wamekuwa walilalamika kuathiriwa na shughuli itokanayo na uoshwaji wa vyombo
vya usafiri mto Mpanda ni pamoja na wakazi wa Kata ya Itenka Halmshauri ya
Wilaya ya Nsimbo Wilayani Mpanda.
Habarika zaidi na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments