WANAUME WATAJWA KUWA MIONGONI MWA SABABU ZINAZOCHANGIA KUONGEZEKA VVU KATAVI
Na.Richard
Sokoni-Mpanda
Imebainika
kuwa ongezeko la maambukizi ya virus vya ukimwi (VVU)
kunatokana na baadhi ya mwanaume kutojitokeza kupima afya zao sanjari na wenzi
wao .
Hayo
yamesemwa na Afisa tathmini wa mipango na ufutiliaji wa maambikizi ya ukimwi
pamoja na magonjwa sugu katika shirika la shdepha mpanda Michael Kapipiti
wakati wa mahjiano na mwandishi wetu ofisini kwake kuhusiana na mwamko wa jamii
kuhusu kupima afya zao .
Aidha Bw.Kapipiti
amesema kuwa baadhi ya wanaume bado hawana elimu ya kutosha kuhusu maambukizi
ya virusi vya ukimwi na ukimwi wenyewe jambo ambalo linasababisha ongezeko la
maambukizi ya ukimwi katika jamii.
Sanjari na
hayo Bw. Kapipiti amesema kuwa wazazi na walezi wanapaswa kutoa elimu
katika familia zao ili kuwa na uelewa
sahihi kuhusu maambukizi ya virus vya ukimwi
na ukimwi wenyewe
Mmoja wa
wakazi wa kata ya Makanyagio Bw. Kulwa Mabula amekiri baadhi ya wanaume kutokuwa na desturi ya
kupima na kujua afya zao.
Mpaka
sasa Mkoa wa Katvi takwimu ya maambukizi kwa mjibu wa tafiti za mwaka 2011/2012
ni asilimia 5.9 ambapo kuanzia kipindi hicho cha tafiti mpaka sasa inakisiwa
idadi ya waathirika kuongezeka kutokana na idadi ya watumiaji dawa ya kufubaza
VVU kuongezeka katika vituo vya afya vinavyotoa huduma hiyo.
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo-Mpanda
Habarika zaidi na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments