MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AKAZA MWENDO KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA WILAYA YAKE
Na.Issack Gerald Bathromeo-Tanganyika
Mkuu wa
wilaya ya Tanganyika Mh.Saleh Muhando ameahidi kulishughulikia swala la mgogoro
wa ardhi katika eneo la Lyamgoroka eneo ambalo linaonekana kuwa limeuzwa na mwenyekiti wa kijiji hicho kinyume cha sheria ya ardhi.
Mkuu huyo wa
wilaya amesema tayari serikali yake imeshachukua hatua ya kuwahamisha watu
ambao walikuwa wakiishi katika eneo hilo kinyume cha sheria kwa kuwatafutia
maneo mapya ya kuishi.
Aidha mkuu
wa wilaya ya Tanganyika amewataka watumishi wote wa wilaya ya Tanganyika kuwa
wadirifu punde wanapotoa huduma kwa jamii bila kupokea au kutoa rushwa kwani
rushwa ndio adui namba moja wa maendeleo .
Katika hatua
nyingine amewataka wafanyakazi wanaohodhi ardhi kinyume cha sheria kuacha mara
moja kwani uongozi wa wawmu hii ni tofauti na wanatakiwa wasome alama za nyakati
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo-Mpanda
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments