HALMASHAURI YA WILAYA MPANDA KUWAWEZESHA WATU WENYE ULEMAVU MWAKA FEDHA 2018/2019
Halmashauri
ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imesema kuanzia bajeti ya mwaka wa fedha
2018/2019 itaanza kutoa asilimia 2 ya mikopo kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
Hatua
hiyo imebainishwa na Kaimu Mkurugenzi
halmashauri hiyo Samson Medda ambapo amesema katika mgawanyo wa asilimia
10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri wanawake watakuwa wanapata asilimia 4 na
vijana asilimia 4 na 2 kwa watu wenye ulemavu.
Kwa
mjibu wa Medda,mpaka kufikia mwezi machi mwaka huu,halmashauri imetoa fedha
kutoka katika mapato ya ndani kiasi cha
shilingi milioni 119 kwa ajili ya kuwezesha vikundi vya wanawake na vijana.
MAENEO AMBAYO HALMASHAURI ILIWEZESHA
1.Kikundi cha
vijana Kata ya Majalila cha kufyatua tofali kilipewa pesa
2.Kikundi cha wanawake
cha Sibwesa kinachoseketa mashuka na vikoi kilipewa fedha
3.Mashine ya
kukoboa na kusaga mahindi-kata ya Kabungu
4.Kiwanda cha
Chaki na Sabuni-kata ya Ifukutwa
5.Pikipiki 11
zilinunuliwa na kusambazwa vijana ambapo 4-zilipelekwa kwa vijana wa Kata ya mpanda
Ndogo,2-kata ya Kapalamsenga,5-kata ya Majalila.
6.Mashine ya
kukoboa Mpunga-kata ya Sibwesa
7.Sakosi ya
Akina mama inayojumuisha wanawake kutoka Katumba,Sibwesa & Kasekese-walipewa
Shilingi milioni 30.
Aidha
ametoa wito kwa idara za maendeleo ya
jamii kutoa elimu ya kutosha kwa
wanawake na vijana wajiunge katika vikundi
ili wanufaike na asilimia 10 inayotengwa na halmashauri.
Hata
hivyo amesema bado kuna changamoto ya urejeshaji wa fedha wanazozikopesha kwa
vikundi mbaimbali vya wajasiliamali.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments