ACT-WAZALENDO WAINGILIA KATI MIGOGORO YA ARDHI KATAVI
Viongozi wa Mkoa wa chama cha
ACT-Wazalendo wakiwa na viongozi wa kata ya Sitalike,wamefika Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga kwa ajili ya kutafuta
mwafaka wa mashamba na mazao ya wananchi katika kata hiyo.
Mwenyekiti wa chama hicho Bw.John
Malack akiwa na Katibu wake Bw.Joseph Mona Mkuu wa Mkoa wakizungumzia hatua
hiyo jana mara baada ya kutoka katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wamesema wamefikia
hatua hiyo kama sehemu ya kusimamia maslahi ya wananchi kwa kuwa ni wajibu.
Aidha wamesema wataendelea kufanya
hivyo na kutafuta tafsiri za kisheria kuhusu migogoro ya ardhi inayoendelea
katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Katavi.
Baadhi ya wananchi wa kata hiyo ambao
wameambatana na ujumbe wa ACT-Wazalendo pamoja na mambo mengine wamesema
wameridhishwa na majibu ya Mkuu wa Mkoa huku
mwenyekiti wa kijiji cha Sitalike Bw.Christopher Mrisho akisema wananchi
wapatao 3500 wa vitongoji vya situbwike,Makutanio na Mgorokani wameathiriwa
zaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga amekiri kuwaruhusu wakazi walioondolewa
katika makazi yao kuvuna mazao yao huku akisema atapanga ratiba ya kwenda
kufanya Mkutano wa hadhara ili kuzungumza na wananchi.
Hata hivyo baadhi ya wananchi
wameendelea kukosa sehemu ya kujenga makazi na kuendesha shghuli za kilimo licha
ya serikali kusema imetenga hekari zaidi ya 7000 kwa ajili ya wakazi hao ambapo
kwa upande wa wananchi bado wanadai hawajaelekezwa hekari hizo zinakopatikana.
Oparesheni ya kuwaondoa wakazi hao
wanaodaiwa kuvamia maeneo ya hifadhi ilifanyika Mwezi Agosti mwaka 2017.
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments