WATOTO WA KANISA KATOLIKI WATOA MSAADA KWA WAGONJWA HOSPITALI YA MANISPAA YA MPANDA
Katika kuadhimisha Alhamisi kuu
kuelekea sikukuu ya pasaka,Watoto wa shirika la mtoto yesu kutoka jumuiya mtakatifu
Filomena kigango cha Kawajense Majengo Mapya jimbo katoliki la Mpanda Mkoani
Katavi,wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa waliopo katika Hospitali
ya Manispaa ya Mpanda.
Wakizungumza kwa niaba ya watoto
wenzao Sesilia John Enock na Samweli wamesema wameamua kutoa msaada kwa wagonjwa
wenye uhitaji ikiwa ni kuadhimisha Alhamisi kuu katika kuelekea sikukuu ya
pasaka.
Jimbo Katoliki la Mpanda Katavi(PICHA NA.Issack Gerald) |
Kwa upande wake Katekista Joseph Paul
Kansato ambaye pia ni mwalimu wa parokia ya kanisa kuu jimbo la Mpanda amesema
watoto hao wametoa misaada mbalimbali ikiwemo sabuni, mafuta na sukari kama
ishara ya upendo walionao kwa watu wenye shida mbalimbali.
Kwa upande wao baadhi ya wagonjwa
wakiwemo Mussa Paul na Magreth Peter Ndekeja wametoa shukrani zao kwa watoto
hao waliotoa msaada huo huku wakiomba jamii kuiga mfano uliooneshwa na watoto
hao.
Miongoni mwa wodi ambazo
wamezitembelea ni pamoja na wodi ya watoto,akina mama,majeruhi pamoja na wenye
uhitaji maalumu.
Maadhimisho ya Alhamisi kuu kuelekea
sikukuu ya pasaka Jumapili ya Aprili mosi mwaka huathimishwa na wakristo kote
duniani kwa kutekeleza amri ya mapendo kama yesu kristo alivyosema.
Habario zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments