WAJASIAMALI KATAVI WASEMA KUHAMIA ENEO JIPYA KUMEWAONGEZEA MAPATO,WAIOMBA SERIKALI KUBORESHA HUDUMA MUHIMU KAMA MAJI ENEO LA KAZI-Julai 19,2017
WAJASILIAMALI
wanaojihusisha na utengenezaji wa vitu vya thamani vikiwemo Vitanda,kabati na
meza waliopo kata ya Misunkumilo
halmashauli ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi,wameiomba serikali
kuboresha miundo mbinu katika eneo hilo.
Baadhi wakiwemo
Florence Vitalisi na Agness Zacharia ,pamoja na mambo mengine wamesema eneo
hilo linakabiliwa na ukosefu wa maji safi na salama kwa ajili ya kunywa na
kupikia hali inayowapa ugumu wa kuendesha shughuli za kibiashara.
Kwa upande wake Katibu wa umoja wa
wajasilimali wanapasifiki Mkoani Katavi Bw.Jastine Mbahi pamoja na kuipongeza
Manispaa ya Mpanda kwa jinsi wanavyowahudumia amesema serikali kutoweka urasmu
na badala yake itemize wajibu wake wa kuhamisha makundi mengine ya
wajasiliamali wahamie katika eneo lililotengwa kama serikali ilivyofanya kwao
ili iwe rahisi kupata wateja na kuinua uchumi wao.
Eneo hilo kwa
sasa lina wajasiliamali zaidi ya 400 waliohamishwa kutoka eneo la Pasifiki Kata
ya Majengo miezi miwili iliyopita ambapo Ofisi ya Mkurugenzi wa manispaa ya
Mpanda ilidai kuwa ni makazi ya watu na hivyo si mahali sahihi kufanyia
shughuli za karakana.
Eneo hilo la wajasiliamali ambalo
lilizinduliwa na mwenge wa Uhuru mwezi Aprili mwaka huu pia linatakiwa kutumiwa
na wenye magari ya kubeba mizigo ambayo hayatakiwi kuwa katikati ya Manispaa.
Bonyeza P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM kwa habari zaidi
Comments