BARAZA LA MADIWANI MPANDA LAONYA WATUMISHI WANAOSABABISHA MIGOGORO YA ARDHI
Na.Issack
Gerald
Baraza la Madiwani Halamshauri ya
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,limesema litachukua hatua kali za kisheria
ikiwemo kuwafukuza kazi watumishi wa idara ya ardhi watakaosababisha migogoro
ya ardhi baina ya wananchi.
Mstahiki Meya wa Manispaa Mpanda Mh.Willium Mbogo |
Amesema kumeanza kujitokeza migogoro
ya ardhi kuhusiana na kiwanja kimoja kuuzwa kwa watu wawili tofauti suala
ambalo limetajwa kufanywa na watumishi wa idara ya ardhi wasio waaminifu na Mstahiki
Meya wa Manispaa hiyo Mh.Willium Mbogo amelazimika kuagiza migogoro hiyo
isuluhishwe wao kwa wao kabla ya tatizo kuwa na baraza kupewa taarifa.
Aidha amesema hatua za kisheria
zitachukuliwa pia kwa watumishi wa idara mbalimbali ambao wamesababisha
Manispaa ya Mpanda Kukosa mapato kutokana na uzembe wao katika uwajibikaji.
Katika Kikao hicho cha siku
mbili,mambo mbalimbali yamejadiliwa katika rasmu ya bajeti ya mwaka wa fedha
2018,2019 ikiwemo masuala ya elimu,afya,miundombinu ya barabara pamoja na
ukusanyaji wa mapato ya halmashauri.
Habari zaidi ni
kupitia P5TANZANIA LIMITED
Comments