RAIS MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI WAPYA NGAZI YA WIZARA NA MIKOA,ABADILISHA WAKUU WA MIKOA GHAFLA
Na.Issack
Gerald-Dar es Salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha
Makatibu Wakuu wapya,Naibu Makatibu Wakuu wapya na Wakuu wa Mikoa wapya sita.
Rais
Mgaufuli mara baada ya kuwaapisha walioteuliwa ,amewaagiza walioapishwa kutatua
matatizo ya wananchi kwa wakati bila kusubiri kusukumwa.
Katika
hatua nyingine,rais Magufuli amefanya mabadiliko ya ghafla akiwa ikulu wakati
akiwaapisha walioteuliwa,ambapo Bi.Christine Solomon Mndeme
aliyetakiwa kuwa mkuu wa Dodoma atakuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma.
Aidha
aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt. Binilith
Mahenge,ameteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Dodoma akichukua nafasi ya Christine
Solomon Mndeme aliyetakiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Wakati
huo huo Rais Magufuli amesema shilingi bilioni 147 alizoidhinisha kwa ajili ya
mikopo ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu,zitolewe kama inavyotakiwa kwa
wakati na pia kwa wanafunzi wenye sifa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au
ukurasa P5Tanzania Limited
Comments