MBUNGE JIMBO LA NKASI KUSINI ATAKA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA JIMBONI KWAKE,SERIKALI YAMJIBU
Na.Issack Gerald-Dodoma kuhusu (Rukwa)
SERIKALI imesema mwaka wa fedha 2015/2016 ilitenga Shillingi
million 300 kwa ajili matengenezo na ujenzi wa Barabara ya Kitosi- Wampembe
katika Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) ili
kufanya Barabara hiyo iweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka.
Serikali imetoa jibu hilo wakati wa swali la Mheshimiwa Mbunge Desdelius
John Mipata Mbunge wa Nkasi Kusini ambaye ametaka kufahamu mikakati ya serikali ya kilio cha wananchi wanaopata shida kwa Barabara hizo
kutopitika katika kipindi chote cha mwaka.
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani
amesema Serikali kupitia Wizara yake imesikia kilio cha wananchi wa Wilaya ya
Nkasi na inaendelea kutoa fedha za matengenezo ya Barabara ya Kitosi-wampembe.
Ukarabati wa barabara ya Kitosi-Wampembe yenye urefu wa kilomita 67 na
Barabara ya Nkana –kala yenye urefu wa kilometa 68 uko chini ya Mfuko wa
Barabara ikisimamiwa na Wakala wa Barabara (TANROADS) na Barabara zote ziko
chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.
Comments