UKAWA WAMPITISHA RASMI LOWASSA KUGOMBEA URAIS WA TANZANIA


 
Edward Lowassa Mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema kupitia Ukawa
NA MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM
Chama cha demokrasia na maendeleo chadema  leo kimemuidhinisha Edward lowasa kuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika  mwezi Oktoba mwaka huu.
 Wajumbe wa mkutano mkuu wa chadema uliofanyika  leo Jijini  Dar Es salaam wamepiga kura ya  kuridhia kiongozi huyo aliyejiunga na upinzani akitokea chama tawala CCM kuwa mgombea  Kiti hicho cha  urais  Kupitia chama hicho.
 Mwanasiasa huyo Mkongwe hapa Nchini amekuwa  akiyagawa  maoni ya Watanzania tangu akihame chama cha Mapinduzi na Kuhamia chama cha  chadema  tangu vikao vya uteuzi vya ccm  kumpitisha mgombea wa urais kulikata jina lake.
Hata hivyo katibu mkuu wa chadema Wilbroad Slaa hakuhudhuria mkutano huo mkuu Kutokana na kuwepo kwa taarifa kuwa hakufurahishwa  na uamuzi wa chadema kumpokea Lowasa.



SOMA HAPA KUMFAHAMU LOWASSA

Edward Ngoyai Lowassa
Edward Ngoyai Lowassa
Edward Lowasa (cropped).jpg

Mbunge
Bunge la
Jimbo la uchaguzi
Monduli (Arusha)
Tarehe ya kuzaliwa
26 Agosti 1953
Chama
CHADEMA (tangu 28/07/15)
Tar. ya kuingia bunge
tangu 1990
Alirudishwa mwaka
2005

Alingia ofisini
2005
Alitanguliwa na
Dini
Mkristo
Elimu yake
Chuo Kikuu
Digrii anazoshika
MA (Development Studies) University of Bath (Uing.)
Kazi
mwanasiasa
Edward Ngoyayi Lowassa (amezaliwa 26 Agosti 1953) ni mwanasiasa nchini Tanzania.
Alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa kumi wa nchi hiyo tarehe 30 Desemba 2005 akajiuzulu tarehe 7 Februari 2008 kwa kutajwa katika kamati ya bunge ya uchunguzi katika utoaji wa tenda kwa kampuni ya umeme ya Richmond kutokana na uzembe wa watendaji walio chini yake.
Lowassa ni mwenyeji na alikuwa mbunge wa Monduli katika Mkoa wa Arusha.
Alisoma shahada ya kwanza katika mada ya tamthilia kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, halafu shahada ya pili katika sayansi ya maendeleo ya jamii kwenye Chuo Kikuu cha Hull nchini (Uingereza).
Mnamo tarehe 28 Julai 2015 alijunga rasmi na chama cha upinzani cha CHADEMA. Hiyo ni baada ya kukatwa jina lake katika kinyang'anyiro cha Urais kupitia chama tawala cha Chama cha Mapinduzi.
Yaliyomo
Nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika
Lowassa ni mwanasiasa mkongwe mwenye uzoefu mbalimbali katika siasa za nchini Tanzania. Lowassa amewahi kushika vyeo mbalimbali katika serikali ya Tanzania kama vile:
Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (2005 - 2008)
Tarehe 29 Desemba 2005 Lowassa aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya kuthibitishwa na bunge na kula kiapo, mchakamchaka wa kuwaletea Watanzania maendeleo ukaanza. Nidhamu, utiifu na uwajibikaji vikaongezeka miongoni mwa watumishi wa umma na viongozi waandamizi, serikali ukarudisha sura yake ya serikali maana viongozi waandamizi wakiwemo mawaziri walijua yupo mtu makini na jasiri wa kuuliza juu ya uwajibikaji wao.
Kazi ya kuboresha shughuli za maendeleo ya jamii zikaanza, moja kubwa ikiwa ni kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa kuanza elimu ya msingi anapatiwa nafasi na kila aliyefaulu kwenda sekondari pia kupatiwa nafasi. Anasifiwa kwa kusimamia kikamilifu kazi ya kuhimiza ujenzi wa sekondari za Kata na nyumba za walimu nchini Tanzania.
Serikali ya awamu ya nne ilianza kwa mitihani mikubwa matatu, wa kwanza ulikuwa na upungufu mkubwa wa chakula ulioikumba baadhi ya mikoa na kutishia  maisha ya wananchi, wa pili ulikuwa ni wimbi kubwa la kutumia silaha hasa kwenye mabenki na wa tatu ni upungufu mkubwa wa uzalishaji wa umeme uliotokana na kushuka kwa kiasi kikubwa cha maji katika bwawa la mtera na kutishia nchi kuingia gizani.
Waziri Mkuu Mhe Lowassa akiwa msimamizi mkuu wa kazi za serikali na mwenyekiti wa kamati ya kushughulikia maafa alimuhakikishia Raisi kwamba pamoja na kuwepo tatizo la upungufui mkubwa wa chakula hakuna mtanzania atakayekufa kwa njaa, Uthibitisho huo wa Waziri Mkuu ukampa nguvu kiongozi wa nchi Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kulitangazia taifa kuwa hakuna atakayekufa kwa njaa. Mhe Lowassa alisimamia kazi ya kutafuta chakula kile kona ya nchi yetu na nje ya nchi na kukipeleka sehemu zenye mapungufu hadi hali ilipokuwa shwari. Sambamba na kukabili upungufu wa chakula katika ushiriki na ushauri wa karibu wa waziri Mkuu kuhusu  masuala ya usalama serikali iliweza kudhibiti wimbi kubwa la ujambazi liliokuwa limezuka.
Hatua muhimu iliyochukuliwa na Serikali katika kukabili tatizo la upungufu wa nishati ya umeme ilikuwa ni kuchukua hatua za haraka kupitia Tanesco kutangaza na kupata mzabuni wa kuzalisha umeme wa dharura ili kuokoa tishio la nchi kuingia gizani. Baada ya Tanesco kupitisha zabuni ya kampuni ya Kimarekani na baada ya kampuni hiyo kushindwa kufanya kazi na kuhamishia mkataba wake kwa kampuni ya DOWANS hapo ndipo sinema ya kisiasa ilipoanza.
Sinema ya Richmond ambayo imekuwa ikijulikana kama sakata la Richmond ilianzia katika kuunda kwa tume ya kuchunguza mchakato wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura, tume hiyo ilidai kampuni ya Richmond  ilianza katika kuunda kwa tume ya kuchunguza mchakato wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura, Tume hiyo ilidai kampuni ya Richmond ilikuwa ni kampuni ya mfukoni, jambo ambalo inawezekana lina ukweli maana hata kabla ya tume kuundwa Waziri Mkuu Edward Lowassa alipata shaka na kampuni hiyo pale iliposuasua kutekeleza mradi na akawa ameshauri mkataba na kampuni hiyo uvunjwe lakini ushauri wa mtaalamu na wanasheria ulitaka serikali ivumilie.
Tume ilidai viongozi wa serikali wa wizara husika na Waziri Mkuu walikuwa wakihimiza Tanesco kukamilisha mchakato wa kumpata mzabuni haraka, jambo ambalo hakikuwakosha maana ni jamba ambalo lilikuwa kwenye mujibu wao kuona nchi haiingii gizani kwa manufaa ya kiuchumi na kiusalama. Pia ni vyema ieleweke pia kwa umuhimu wa umeme kiuchumi na kiusalama suala la kupata mitambo ya kufua umeme wa dharura lililozungumzwa na kupata vikao vyote muhimu vya serikali ngazi ya Taifa likiwemo baraza la mawaziri.
Sinema zaidi ya kisiasa ilikuja kubainika katika mambo makubwa matatu; Kwanza ni kumtaka Waziri Mkuu apime na anatakiwa kuwajibika katika jambo ambalo halibainishi kosa lolote kwake, kiutawala wala kisiasa. Mbili mabishano ya wanasiasa juu ya kutumia au kutoendelea kutumia mitambo ya DOWANS, na tatu mabishano ya wanasiasa juu ya kulipwa au kutolipwa  kwa kampuni ya DOWANS.
Ili kulinda heshima ya serikali nzima, Chama tawala CCM na pia ili kuepuka mgawanyiko miongoni mwa wanachama, wananchi na viongozi Lowassa aliamua kujiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu. Wabunge wa CCM waliokutana kama kamati kuzungumza suala hili zaidi ya asilimia 80% walitaka Waziri Mkuu Lowassa asijiuzulu kwa kuwa hausiki na chochote. Na kwa upande wa kamati ya bunge, mwenyekiti wa kamati hiyo Harrison Mwakyembe, mnamo tarehe 15 February 2008 alikiri kuwa, Edward Lowassa alijiuzuru kwa makosa ya watendaji wa chini yake.
Kuhusu hoja ya kulipwa DOWANS na kuendelea kutumika kwa mitambo ambayo ililetwa na DOWANS jambo hili lilikwenda kwenye mabaraza ya kimataifa na kuonekana wana haki ya kulipwa na mitambo iliyodaiwa na wanasiasa kuwa haifai ndiyo inayoendelea mpaka leo kufua umeme na Raisi ya Marekani Baraka Obama katika ziara yake hapa nchini aliitembelea na kusema ni moja ya mitambo bora sana katika bara la Afrika, lakini kwa wanasiasa bado sinema bado inaendelea.
Waziri wa Maji na Mifugo (2000 - 2005)
Mwaka 2000 – 2005 alikuwa waziri wa maji na maendeleo ya mifugo. Mwanamapinduzi Edward Ngoyai Lowassa aliitumia tena nafasi kutekeleza jukumu alilokuwa amepewa na taifa kwa kuweka na kusimamia mikakati ya kuhakikisha maeneo ya vijiji vyetu vinapata maji kama sera ya CCM ilivyoelekeza, Hata hivyo alikerwa na matatizo mawili makubwa, moja lilikuwa ni kampuni ya iliyokuwa na imeingia mkataba na serikali kusambaza huduma za maji (city water) kushindwa kutekeleza wajibu wake na la pili lilikuwa ni tatizo la maji katika mkoa wa Shinyanga na baadhi ya mkoa wa Mwanza.
Kwa kuwa Lowassa hana tabia ya kulalamika wala kusikitika bali kuchukua hatua za kutafuta ufumbuzi, Mwanamapinduzi huyu aliamua kufanya maamuzi magumu lakini muhimu kwa kuvunja mkataba na city water, uamuzi ambao aliusimamia pamoja na kuwepo kwa mikono ya watanzania wenzetu waliotaka city water waendelee kubaki ili wao wanufaike. Uamuzi huu ulileta huzuni kwa watumiaji wa maji katika jiji la Dar ingawa changamoto bado zipo hasa kutokana na ongezeko kubwa la watu na ujenzi wa maeneo mapya katika jiji.
Zaidi ya hilo la city water waziri Lowassa aliamua kuchukua hatua za kupanga na kuishawishi serikali kuingia katika mradi mkubwa wa kutoa maji katika ziwa Victoria na kuyasambaza katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga, huu ni miongoni mwa miradi michache mikubwa iliyotekelezwa kwa kodi za watanzania bila kutegemea ufadhili aidha pia ni mradi uliowasaidi wananchi wengi katika maeneo bomba hili lilipopita na moja ya manufaa makubwa ni kupungua kwa kwa magonjwa yaliyotokana na utumiaji wa maji yasiyo salama.
Waziri wa ardhi na makazi (1993 - 1995)
Akiwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Mijini, Lowassa alisimamia utekelezaji wa mkakati wa upimaji viwanja kwa maendeleo ya miji na kupambana na tatizo lililokuwa limeanza kuota mizizi la kuwagawia watu zaidi ya mmoja kiwanja kimoja.
Wale wakazi wa jiji hawatasahau uamuzi mzito na mkubwa wa kufatia maamuzi ya  Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ya kumgawia mfanyabiashara mmoja eneo la uwanja wa kumbukumbu ya Uhutu (Mnazi Mmoja) ili ajenge vibanda vya biashara. Uamuzi huu wa Mhe Waziri Lowassa aliungwa mkono na vijana wanaofanya biashara mitaani (machinga) na wakaandamana na kwenda kuvunja uzio wa mabati uliokuwa umewekwa na mfanya biashara huyo katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Uamuzi huo wa Waziri Lowassa ulizingatia kulinda heshima na hadhi ya Serikali na zaidi ulizingatia kuwa matumizi ya viwanja vya mnazi mmoja ni kwa ajili ya shughuli za umma na wananchi wanapaswa kuwa huru kuutumia na kuangalia shughuli zinazofanyika bila kizuizi. Maamuzi ya aina hiyo hufanya na watu wenye uzalendo na utaifa.
Nyadhifa nyinginezo
  • Waziri mdogo wa haki na mambo ya bunge katika ofisi ya Makamu wa Rais (1990-1993)
  • Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (1989 - 1990)
  • Waziri mdogo wa mazingira na mapambano dhii ya umasini katika ofisi ya Makamu wa Rais (1988-2000)
  • Mbunge wa Monduli tangu 1990
Uchaguzi mkuu 1995
Mwaka 1995 Edward Lowassa aliamua kuingia katika mchakato wa kumpata mgombea uraisi kwa tiketi ya CCM, Wakati huo Lowassa aliombwa na Umoja wa Vijana kupitia kikao cha baraza kuu la Taifa achukue fomu akiwa miongoni mwa wana CCM wanne ambao vijana waliamini wamaweza kuliosaidia Taifa kupiga hatua za haraka kuelekea kwenye maendeleo endelevu, wengine waliokuwa waliokuwa wametajwa na Umoja wa vijana ni pamoja na Salim Ahmed Salim, Laurance Gama na jaji mstaafu Mark Bomani.
Katika hatua ya kuchagua majina matatu kati ya majina 11 yaliyoomba nafasi jiyo Lowassa akawa hakupendekezwa, lakini hakununa wala kususa bali aliamini kuwa Mwanamapinduzi mwenzie Jakaya Mrisho Kikwete ataweza kutekeleza dhamira aliyokuwa nayo ya kuwaletea watanzania maendeleo, hivyo alirudi kwa makundi mbalimbali wakiwemo vijana wa CCM ambao walihoji kwanini ameengeliwa na yeye kwa utii mkubwa kwa CCM aliwataka vijana na viongozi wengine waheshimu maamuzi ya chama na kumuunga mkono Jakaya M Kikwete. Ikumbukwe kuwa mwana-CCM mwingine aliyekuwa anakubalika kwa umma Lowassa aliamua kuondoka mapema kuondoka CCM kwa sababu ndogo tu ya kubadilishwa wizara na kuamua kwenda chama cha NCCR mageuzi ambako aligombea uraisi kwa chama hicho na kuleta upinzani mkubwa.
Yapo maneno ya baadhi ya wanasiasa kwamba kurtoteuliwa kugombea kwa Mhe Lowassa kulitokana na kuonekana anamiliki fedha nyingi akiwa na muda mfupi kwenye utumishi  wa umma, lakini pia inasemekana kuwa wale waliohoji kukatwa kwa jina lake kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya |Taifa majibu yalikuwa, CCM iliamua kupeleka majina matatu kwenye mkutano mkuu ili wachague moja katika uwakilishi huo wa majina walipenda apatikane mtu  mzima mmoja, mwenye umri wa kati mmoja na kijana mmoja, watu hao ni mzee David Msuya ambae ni mtu mzima, Benjamini Mkapa ambae umri wake ulikuwa wa kati na kijana ambae ni Jakaya Kikwete.
Lakini maneno hayo ya baadhi ya wanasiasa hayakuishia hapo wakadai baada ya Rasi Mkapa kuchaguliwa hakumteua Mhe Lowassa kwa kuwa aliagizwa na Mwalimu Nyerere asimteue mpaka achunguzwe kama uwezo kiasi wa fedha alionao untokana na mapato halali, siyo halali asimteue. Mwaka 1997 Rais Mkapa akamteua Lowassa kuwa Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais mazingira. Maneno hayo ya baadhi ya wanasiasa ni ya ukweli basi uchaguzi ulifanyika na kuonekana mapato yake ni halali au vinginevyo unaweza kusema ni hisia za kimazingira.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA