MADIWANI WATATU CHADEMA WASIMAMISHWA
Madiwani watatu wa CHADEMA halmashauri ya Mji wa Njombe wametolewa
nje ya kikao cha baraza la madiwani na kusimamishwa kuhudhuria vikao 3 kutokana
na kujadili mkataba wa halmashauri na kampuni iliyowekwa kukusanya ushuru
ambayo inawanyanyasa wananchi.
Madiwani hao ni pamoja na George Sanga diwani Kata Ramadhani,Sigrada
Mligo,diwani viti maalum,Legnard Danda diwani kata Ihungilo.
Madiwani hao walitolewa kwenye mkutano na kusimamishwa
kuhudhuria vikao vitatu baada ya kuhoji mkataba wa halmashauri na kampuni ya
Ihagara inayo kusanya ushuru mjini Njombe ambayo inadaiwa kuwanyanyasa
wananchi.
Awali
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Njombe, Edwin Mwanzinga alipiga marufuku
kujadili suala hilo kwa madai kuwa baraza halina mkataba huo na hakuna palipo
andikwa jina la kampuni hiyo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments