MKOA WA KATAVI KUUNGANISHWA NA GRID YA TAIFA
WAZIRI wa Nishati Dr.Merdard Kareman amesema miaka miwili ijayo shirika la umeme Tanesco mkoani Katavi litakuwa limeunganisha Mkoa wa Katavi katika gridi ya taifa.
Waziri Kareman ametoa kauli
hiyo wakati akikagua mradi
wa mashine za kuzalisha umeme katika mji wa Inyonga wilayani.
Amesema
mpaka kufikia mwaka 2019 maeneo mengi hasa vijijini yatakuwa yameunganishwa na
umeme ili kuongeza kasi ya uchumi wa viwanda mkoani Katavi.
Kwa sasa Mkoa
wa Katavi unatumia jenereta kuzalisha umeme unaotumika ktika wilaya za
Mpanda,Mlele na Katavi ambapo wakazi wengi wamekuwa wakilalamikia tatizo la
umeme jenereta linapokuwa na tatizo.
Waziri Kareman ambaye
alifanya ziara Mkoani Katavi akitokea Mkoani Kigoma aliendelea na ziara Mkoani
Rukwa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA
LIMITED
Comments