SHIRIKA LA WORLD VISION KUKABIDHI VIFAA TIBA KWA VITUO VYA AFYA 111 MKOANI
Na.Isaac
Isaac-Kigoma
Jumla
ya vituo vya afya 111 vintarajiwa kunufaika kwa kupatiwa vifaa tiba pamoja na
ujenzi wa wodi na vyumba vya upasuaji katika wilaya tatu (3) za mkoa wa Kigoma.
Kigoma Ujiji |
Kauli
hiyo imetolewa na meneja mradi Monica Dedu kutoka katika shirika la world Vision
wakati wa semina elekezi kwa viongozi wa madhehebu ya kidini pamoja na
madiwani katika Manispaa ya Kigoma ujiji
ili kutia moyo na kuhamasisha jamii
kuona umuhimu wa kutumia huduma za afya.
Naye
Mganga mkuu wa mkoa Kigoma Poul Chaote amesema asilimia 65 ya akina mama
wajawazito ndio wanaofika katika vituo vya afya kwa ajili ya kujifungua huku
wengine wakijifungulia majumbani jambo linalohatarisha afya zao lakini pia
usalam wa maisha ya watoto
Kwa
upande wao baadhi ya viongozi wa kidini wamesema serikali bado ina jukumu la
kuweka miundo mbinu bora katika maeneo
ya vijijini kwa kuwa ndio sehemu ambazo kuna kiwango kikubwa cha vifo vya
akina mama na watoto ambapo wamesema jambo hilo litasaidia kupunguza vifo vya
akina mama wajawazito na watoto mkoani kigoma.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments