SERIKALI IMEANIKA SABABU ZA KUJITOA OGP,ATISHIA KUFUTA BARAZA LA MADIWANI KIGOMA MJINI
Serikali imekiri kujitoa kwenye Mpango wa Kimataifa wa
uendeshaji wa shughuli za serikali kwa uwazi (OGP), ambao serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ilijiunga Septemba 21 mwaka 2011.
Mh.George Mkuchika |
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na
Utawala Bora,Mh.George Mkuchika wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini
Mh. Zitto Kabwe lililohoji kwanini serikali imejitoa kwenye Mpango wa Kimataifa
wa uendeshaji serikali kwa uwazi (OGP).
Mh.Mkuchika amesema baada ya serikali kushiriki kwenye
utekelezaji wa mpango huo kwa muda wa miaka minne imeamua kujitoa ambapo
ameongeza kuwa sio nchi ya kwanza kujitoa kwenye mpango huo.
Kwa upande mwingine Mh.Zitto ameshauri kuwa serikali ingeendelea
kuwa mwanachama wa (OGP) ingefaidika kwa sulaa la ndege za Bombadier ambazo
zimekwama nchini Canada kutoka na nchi hiyo kuwa ndiyo mwenyekiti wa sasa wa
OGP.
Hata hivyo Waziri amesisitiza mahusiano ya Tanzania na Canada ni
mazuri bila hata ya Tanzania kuwa mwananchama wa (OGP) ambapo masuala ya
Bombadier yatashughulikuwa na balozi wa Tanzania nchini humo.
Mpango wa kuendesha serikali kwa uwazi ulizinduliwa Septemba 20
mwaka 2011 na rais wa zamani wa Marekani Barack Obama ikiwa kama taasisi
binafsi.
Waziri Mkuchika ameionya Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma kuendelea
na mawasiliano na washirika wa OGP baada ya Tanzania kujitoa ambapo amesema
wakifanya hivyo atafuta baraza na kuweka uongozi mwingine unaokuwa na tume.
Hadi sasa umoja huo una nchi wanachama 70 ambapo nchi 10 pekee
ndio zinatoka barani Afrika.
Habari zaidi ni P5TANZANIA
LIMITED
Comments