LULU AHUKUMIWA JELA MIAKA 2 KWA KESI YA KUUA
Na.Issack Gerald
Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemhukumu
kwenda jela miaka miwili muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael (Lulu)
ambaye alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia.
Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji Sam Rumanyika aliyekuwa
anaendesha kesi hiyo na kusema mshtakiwa amekutwa na hatia ya kuua bila
kukusudia kutokana na ushahidi wa mazingira,hivyo atatumikia kifungo cha miaka
miwili jela.
Baada ya hapo jaji rumanyika aliwapa nafasi upande wa mshtakiwa
kujitetea ambapo wakili wake Peter Kibatala alimtetea mshakiwa kwa kusema mshtakiwa
anategemewa na familia yake.
Mara baada ya utetezi huo,Jaji Rumanyika alitoa
hukumu yake na kumuamuru mshtakiwa kwenda jela kwa miaka miwili.
Elizabeth Michael (Lulu) anahukumiwa kwa kumuaa aliyekuwa mpenzi
wake Steven Charles Kanumba ambaye pia ni muigizaji mwenzake,mnamo April 7,
2012.
Habari zaidi ni P5TANZANIA
LIMITED
Comments