BAADA YA HUKUMU YA LULU,MAMA WA MAREHEMU KANUMBA AZUNGUMZA
Mama wa Muigizaji Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amesema leo
atakwenda makaburi ya kinondoni alipoziikwa mwanaye ili kumzika upya.
Mama wa Marehemu Kanumba |
Mama Kanumba ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Mahakama Kuu
kumhukumu kifungo cha miaka miwili Muigizaji Elizabeth Michael ambaye alikuwa
mtuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia yaliyopelekea kifo cha muigizaji
huyo.
"Kwa sasa sina la kusema ila naishukuru sana Mahakama
kwa kutenda haki, pia niishukuru sana Serikali yangu lakini pia nikitoka hapa
nitakwenda makaburini kwa ajili ya kumzika upya mwanangu Kanumba". Mama Kanumba
Kwa upande wa
Wakili wa Muigizaji Lulu Peter Kibatala ameweka wazi kwamba watakata rufaa
kufuatia hukumu ya Mahakama iliyotolewa leo kwa mteja wake.
Muigizaji Lulu
leo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya
kumuua muigizaji mwenzake ambaye pia alikuwa mpenzi wake Steven Kanumba usiku
wa Aprili 7 2012.
Habari zaidi ni P5TANZANIA
LIMITED
Comments