AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA YA UCHOMAJI NYUMBA MPANDA
Na.Mgeni
Shabaani-Mpanda
MTU
mmoja mkazi wa tambukareli Kata ya Mpanda Hoteli Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi
amefikishwa katika mahakama ya mwanzo mjini Mpanda akikabiliwa na shtaka la
kuchoma moto nyumba na mali ya Anatalia Golikondwe mkazi wa tambuka reli.
Akisoma
shitaka hilo mbele hakimu
mwandamizi Bw. David |Mbembela,askari wa
jeshi la polisi Bi.Elineema amemtaja mshtakiwa huyo kuwa ni Bw Michael Damas
(40) ambaye alitenda kosa hilo Desemba 19 mwaka jana, majira ya saa 9 usiku.
Amesema
mshtakiwa alichoma nyumba hiyo na kuteketeza mali zilizokuwa ndani ya nyumba
hiyo zenye thamani ya shilingi laki tano kumi na nne elfu.
Aidha
mahakama imepitia ushahidi kutoka upande wa mlalamikaji na imejilidhishana
kuona mshitakiwa ana kesi ya kujibu kwa kanuni na sheria
Hata
hivyo,mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na mahakama imeahirisha kesi hiyo
mpaka itakapo tajwa tena tarehe 29 machi mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza
ushahidi kutoka upande wa mshtakiwa, na
mshtakiwa huyo yupo nje kwa dhamana.
Comments