WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI MPANDA WAKITUHUMIWA WIZI WA FEDHA KWA KUTUMIA SIMU
Na.Issack Gerald-Mpanda
Watu
wawili wakazi wa kijiji cha Ikaka kata
ya Mnyagala wilayani Mpanda mkoani Katavi,wamefikishwa katika mahakama ya
mwanzo mjini Mpanda wakikabiliwa na shtaka la wizi wa fedha kwa njia ya
simu ambayo ni mali ya Charles Lubasha
mkazi wa Kakese.
Akisoma
shtaka hilo mbele ya hakimu mwandamizi Bw David Mbembela,askari wa jeshi la
polisi WP8940 PC Shakira amewataja
washtakiwa hao kuwa ni Bw.Emmanuel Makopo (23) na Cosmas Faustene(33) waliotenda
kosa hilo Machi 7 mwaka huu majira ya saa kumi jioni.
PC
Shakira amesema washtakiwa hao waliiba pesa zenye thamani ya shilingi laki sita
na elfu tano kwa kutumia simu mali ya Lubasha.
Hata
hivyo washtakiwa wamekana kosa hilo ambapo pia polisi imeweka pingamizi ya
dhamana dhidi yao kutokana na kuwa na kesi nyingine mahakamani.
Kufuatia
hatua hiyo,mahakama imeahirisha kesi mpaka itakapo tajwa tena machi 18 mwaka huu.
Comments