WILAYA YA NKASI YATANGAZA VITA DHIDI YA WANAUME WANAORUBUNI WANAFUNZI KUSHIRIKI MAPENZI.
KATIKA kukabiliana na tatizo la mimba kwa wanafunzi wanaume
wilayani Nkasi Mkoani Rukwa wameonywa kuacha mara moja tabia ya
kuwaita watoto hao wa kike majina ya mahaba kwani yanawapelekea kujiona wamekua
na kuanza kushiriki vitendo vya ngono.
Wito huo umetolewa jana na afisa elimu Sekondari wilayani Nkasi
Abel Ntupwa kwenye kikao kazi kilichowajumuisha Wakuu wa shule 23 za
sekondari wilayani Nkasi kilichomshirikisha na afisa elimu wa mkoa
Nestory Mloka kilicholenga kupeana mikakati namna ya kuboresha taaluma baada ya
wilaya Nkasi kuporomoka sana kwenye mitihani ya kitaifa.
Alisema hivi sasa watu wazima wamekua na tabia ya kuwaita watoto
hao wa kike ambao ni Wanafunzi majina ya kimahaba kama Baby kama mzaha na
mwisho wa siku ujikuta Watoto hao wanajiingiza kwenye mtego huo mbaya na hivyo
kuanza kushiriki vitendo vya mapenzi.
Hivyo kufuatia hari hiyo amedai kuwa ni marufuku kwa
mtu yeyote kumwita mtoto wa kike ambaye ni
Mwanafunzi majina hayo ya Baby ili kuwaweka Watoto hao katika
hari ya usalama.
Lakini pia alikemea tabia ya baadhi ya Walimu wenye tabia ya
kujihusisha kimapenzi na Wanafunzi au hata kuwatamani kuwa hakuna dhambi kubwa
kwa Mwalimu kama hiyo na kuwa hakuna atakaebaki salama kwa kujihusisha na tabia
hizo pindi itakapobainika.
Lakini pia aliwataka Wakuu wa shule kuhakikisha kuwa wao ndiyo
wakaguzi wa kwanza katika shule zao kwa kuhakikisha kuwa Walimu wao
wanafundisha sawasawa na kuleta tija ya kitaaluma katika masomo
wanayoyafundisha.
Alisema shule yoyote inayofanya vizuri ni matokeo ya uongozi
bora wa shule ambapo Walimu wakuu wameamua kuzisimamia shule zao na kuwa sasa
wameamua kuboresha elimu wilayani Nkasi nas kutaka Wakuu wa shule kusiomama
imara na kama kuna ambaye atakwenda kinyume na kasi
hiyo watamshughulikia mara moja.
Kwa upande wake afisa elimu wa mkoa wa Rukwa Nestory Mloka
alisema kuwa yeyebinafsi kamwe hawezi kusita kuwavua madaraka Walimu wakuu
ambao wataonyesha kushindwa kuzisimamia shule zao ili zitoe matokeo chanya na
kuwa haoni sababu kwa wilaya Nkasi iliyokuwa inaongoza katika mkoa Rukwa sasa
imeanza kushika mkia.
Alisema kwa kuanza wameanza na mabadiliko madogo ambapo wameteua
baadhi ya waratibu wa elimu kata kutoka katika shule za Sekondari na msingi na
kuwataka washirikiane nao vizuri na kuwa wanataka kuona mwaka huu mabadiliko
yanatokea lakini kinyume cha hapo alisema kuwa hatamuelewa mtu.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments