WATOTO 400 WAKOSA ELIMU WILAYANI SUMBAWANGA
JUMLA ya watoto wa wavuvi wapatao 400 waliopo katika kambi ya
wavuvi ya Nankanga wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa ambao wamefikia umri wa
kuanza darasa la kwanza wameshindwa kupata haki yao ya elimu kutokana na
kutokuwa shule.
Diwani wa kata ya Nankanga wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa,
Anyisile Kayuni alimwambia hayo mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo wakati akiwa
katika ziara ya kukagua makambi ya wavuvi katika suala la kukabiliana na
ugonjwa wa kipindu pindu.
Alisema kuwa watoto hao wanaishi na wazazi wao katika kambi hiyo
ya Nankanga iliyopo katika kijiji cha Nankanga,kata ya Nankanga na wamefikia
umri wa kuanza shule ya msingi lakini wameshindwa kutokana na kuwa katika eneo
walilopo hakuna shule.
Diwani huyo alisema kuwa shule ya msingi ipo umbali wa kilomita
tisa kutoka yalipo makambi hayo umbali ambao ni mkubwa huku ukikabiliwa na
changamoto ya barabara kitendo kinachosababisha washindwe kwenda shule.
alisema kuwa kwa kuliona hilo yeye kupitia uongizi wa makambi
hayo walikubaliana kujenga shule ambapo mbapa sasa wamejenga vyumba viwili vya
madarasa na kufikisha usawa wa lenta ambapo wanaiomba serikali ya mkoa
iwasaidie bati 100 wapaue vyumba hivyo na kuwapelekea walimu ili watoto hao
waanze kusoma.
Alisema kuwa katika kambi hiyo wavuvi waliopo wanajitahidi
kuzingatia huduma za afya bora ikiwamo ni pamoja na kuchimba vyoo, pia wanapata
huduma za dawa za kufubaza virusi vya ukimwi ambapo wapo watu 270 wanaotumia
dawa hizo na wameweka mkakati kuhakikisha kuwa hawaachi kutumia ili waishi
maisha yenye afya na marefu.
Kwaupande wake mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo alifurahishwa na
hatua ya wananchi hao kuanzisha suala la ujenzi wa shule ili watoto hao wapate
elimu ambapo aliahidi ofisi yake itatoa bati 50 na aliigiza halmashauri ya
wilaya hiyo kutoa bati nyingine 50 ili vyumba hivyo vya madarasa vipauliwe na
watoto hao waanze shule mara moja.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments