WAKAZI MKOANI KATAVI WALALAMIKIA KIGEZO CHA NDUGU WA NNE WANAOTAKIWA KUCHANGIA DAMU ILI MGONJWA ATIBIWE



Na.Issack Gerald

Baadhi ya Wananchi mkoani Katavi wamekitaja kitendo cha kutakiwa kuleta ndugu wanne wa kujitolea damu pindi mgonjwa anapo kuwa na tatizo la kuishiwa damu kuwa kikwazo katika  huduma ya afya .

Wamesema hayo kwa nayakati tofauti kueleza kuwa hali hiyo ndiyo inayo chochea vitendo vya rushwa ili kupata huduma

Kwa uapande wake  mratibu  wa damu salama wa hospitali ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi  Khadija Juma  amesema mgonjwa kutakiwa kuwa na ndugu wane ili kurejesha damu iliyotumika kwa mgonjwa wake ni mpango uliopitishwa na serikali.

Bi.Juma amesema kwa mwezi hutumika chupa 350 na Hospitali hiyo inaingiza chupa 400 mpaka 600 hivyo kiwango hicho kinakidhi mahitaji ya wagonjwa.

Aidha amewaomba kujenga tabia ya  kujitolea damu kwa kwa hiari,wakati wote na siku yoyote katika masaa ya kazi.

Wiki iliyopita Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu amezitaka Hospitali na vituo vya Afya nchini kuhakikisha wagonjwa hawauziwi damu na atakayeuza damu hatua za kisheria zitachukuliwa kwa aliyehusika.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA