WALIMU WA SHULE BINAFSI MKOANI KATAVI WAELEZA CHANGAMOTO TAMKO LA SERIKALI KUHUSU VIWANGO VYA UFAULU


Walimu wa shule za sekondari za binafsi mkoani Katavi wameelezea kuwepo kwa  changamoto utekelezaji wa agizo la kuweka kiwango sawa cha ufaulu kwa shule za binafsi na serikali.

Kauli hiyo inakuja kutokana na maagizo ya serikali kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ambapo shule binafsi zimetakiwa kubadilisha mfumo kwa ufaulu wa wanafunzi na kuwa sawa na shule za serikali.

Wamesema itawalazimu kubadilika japo hatua hiyo haitamjenga mwanafunzi kitaaluma kwani wengi wao wanaosomea katika shule binafsi ni wale walioshindwa kufaulu kwenye shule za serikali.

Hatua hiyo ya wizara ya elimu imetajwa kuwa ni moja ya kupunguza upatikanaji wa wanafunzi watakao jiunga na shule binafsi  kwani kutakuwa hakuna umuhimu kutokana na usawa katika viwango vya ufaulu.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

 


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA