TUNDU LISSU AFANYIWA OPARESHENI YA 19 AWASHUKURU WANAOMUOMBEA
Mbunge
wa Singida Mashariki kwa tiketi ya (CHADEMA) Tundu Lissu amefunguka na
kuwashukuru Watanzania kwa maombi yao kwake kufuatia oparesheni nyingine ya 19
ambayo amefanyiwa katika mguu wake.
Tundu
Lissu juzi alifanikiwa kufanyiwa oparesheni hiyo katika mguu wake wa kulia na
kuisha salama,madaktari waliamua kufanya oparesheni hiyo kufuatia kugundua moja
ya mfupa wake ulikuwa ukichelewa kuunga na kudai kuwa kama wasingefanya
upasuaji na kurekebisha mfupa huo ungeweza kuchelewa zaidi na kuja kuvunjika
baadae.
Hata
hivyo Watanzania mbalimbali wameendelea kumuombea Tundu Lissu ili aweze kupona
haraka na kurudia tena katika hali yake ya zamani ili aweze kurudi nyumbani
Tanzania na kuendelea na majukumu yake ya kila siku.
Tundu
Lissu alishambuliwa kwa risasi mnano Septemba 7, 2017 na watu wasiojulikana
akiwa mjini Dodoma na kisha baadae kupelekwa nchini Kenya kwa matibabu ambapo
huku alifanyiwa oparesheni kadhaa katika mwili wake na baadae alikwenda nchino
Beljium kwa matibabu zaidi ambapo jana amefanikiwa kufanyiwa oparesheni ya 19.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments