IFAHAMU TUMBAKU ASILI YAKE,ATHARI KIAFYA,KILIMO MPAKA UVUNAJI NA NCHI ZINAZOONGOZA KILIMO DUNIANI
Asili ya tumbaku
Asili
ya tumbaku ni Amerika ambako Maindio wenyeji waliitumia kama dawa ya
kidini pia ya burudani. Tangu Kolumbus Wahispania walipeleka mtumbaku
hadi Ulaya ambako uliangaliwa mwanzoni kama mmea wa kiganga. Matumizi hasa kwa
njia ya kuvuta na kutafuna yalienea haraka katika Ulaya na kwa njia ya
mabaharia Wareno katika pande zote za dunia.
KAZI YA NIKOTINI NDANI YA TUMBAKU
Tumbaku
inavutiwa hasa kwa sababu nikotini ambayo ni dawa ndani yake inaathiri ubongo
na neva ya binadamu na kupunguza uchovu na kusaidia mtu kusikia utulivu na
raha. Tofauti na madawa mengine kama pombe,bhangi au afyuni yanayoathiri pia
ubongo na neva tumbaku haisababishi hali ya ulevi. Lakini inasababisha haraka
uzoefu wa mwili unaoshikwa na hamu ya kupata nikotini tena na tena. Hapo ni
vigumu kwa watu walioanza kutumia tumbaku mara kwa mara kuachana na matumizi
yake.
HATARI ZA KIAFYA
Matumizi
ya tumbaku yamegunduliwa kuwa kati ya sababu kuu zinazosababisha magonjwa mengi
kwa binadamu pamoja na kansa,magonjwa ya moyo na mapafu,na mengine.
Magonjwa
haya hayasababishwi na nikotini lakini na desturi ya kuvuta tumbaku.
Moshi
ya majani ya tumbaku huwa na maelfu ya kemikali ndani yake ni hasa kemikali
hizi zinazovutwa ndani ya mwili wakati wa kuvuta ambazo ngozi ndani ya
mwili,mishipa,moyo na mapavu.
Kwa
hiyo nikotini inamlazimisha mvutaji kuvuta tena na tena na hivyo kuingiza
mwilini kemikali nyingi zenye hasara.
Matumizi
ya tumbaku nje ya kuvuta (kutafuna,kunusa) yamegundunduliwa kupunguza hatari za
kiafya lakini inaleta matatizo yaleyale ya kutegemea nikotini na kutoachana
nayo.
Nchi
zilizolima zaidi ya tani 100,000 za tumbaku mwaka 2000
Kilimo
cha tumbaku ni tawi muhimu la uchumi kwa nchi mbalimbali. Kilwa mavuno ya
duniani ni takriban tani milioni 6.7. Wazalishaji wakuu ni China (39.6%),Uhindi (8.3%), Brazil(7.0%) na Marekani (4.6%).
Tanzania
ni kati ya nchi kumi za kwanza zinazolima tumbaku inavuna asilimia 1.6 ya
tumbaku ya dunia.
Katika
nchi zilizoendelea kilimo cha tumbaku kimepungua na kiasi cha China
kumeongezeka.
Mavuno
hutokea siku 70 hadi 130 baada ya kulima shamba.
Majani
huvuniwa wakati majani yanaanza kuonyesha rangi ya manjano maana yameiva.
Mavuno
yanaenda kwa uangalifu kwa sababu mashimo katika majani yanapunguza ubora na
bei,Baada ya mavuno majani yanafungwa pamoja kwa kamba na kukaushwa.
Kuna
mbinu za kuzikausha polepole kivulini au juu ya moto au penye hewa ya moto
haraka katika muda wa siku chache tu.
Majani
yaliyokauka hufungwa pamoja kwa mchakato wa kuchachua.
Huu
unabadilisha ladha ya tumbaku kwa njia inayotakiwa. Baadaye tumbaku hutiwa sosi
zenye sukari au vitu vingine vya kutia ladha halafu kukatwa na kufungwa
kulingana na matumizi kama tumbaku ya kuvuta katika sigara za kawaida,sigara
kubwa,pipo,ya kutafunia au ya kunusu.
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments