WALIMU 16 WAFUTWA KAZINI
JUMLA ya walimu 16 wamefukuzwa kazi wilayani Nkasi mkoani
Rukwa kwa kipindi cha miaka mitatu na wengine 11 wamepewa onyo kali baada ya
kubainika wametenda makosa mbalimbali.
Hatua
hiyo imethibitishwa jana na Katibu wa tume ya utumishi wa
walimu TSC wilayani humo Richard Katyega mbele ya kamishina wa
tume ya Utumishi wa walimu Taifa,Samwel Koroso ambapo alisema kuwa katika
kipindi hicho walipokea mashauri 23 na kupelekea walimu 16 kufukuzwa
kazi,11 kupewa onyo kali na wengine 5 waliondolewa kazini baada ya kubainika
kuwa na vyeti bandia.
Alisema
katika mwaka wa fedha wa 2016,2017 na 2018 tume hiyo imesikiliza mashauri
hayo na kuyatolea maamuzi ambapo ilifikia maamuzi hayo baada ya kusikiliza
mashauri hayo na pasipo kumuonea mwalimu hata mmoja na kutenda haki kwa mujibu
wa sheria.
Katyega
alisema tume hiyo sambamba na kuchukua maamuzi hayo pia imekua ikiwahamasisha
walimu kufuata maadili ya ualimu kwa uhakika ili wasiweze kukumbana na adhabu
mbalimbali ikiwemo kufukuzwa kazi kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake kamishna wa tume ya TSC Samwel Koroso
alionyesha kusikitishwa na vitendo vya uvunjifu wa maadili kwa waalimu
hali inaoyopelekea kufukuzwa kazi na kuwa wao kama tume ya maadili kwa
walimu wataendelea kuwachukulia hatua Walimu wote ambao watakwenda kinyume na
maadili ya ualimu.
Aliwataka walimu kwenda sambamba na misingi ya sheria ya
utumishi kwa walimu kama inavyowataka na kuongeza kuwa walimu wilayani humo
hawana budi kuzipitia sheria za utumishi wa walimu ili waishi kwa kufuata
sheria hizo kama zinavyoagiza.
Maofisa kutoka ofisi ya ya kamishina wa tume hiyo nao walikutoa
mada mbalimbali zilizolenga kuwapatia elimu Walimu na kuwakumbusha sheria za
utumishi wa walimu,huku walimu kwa upande wao walipata fursa ya kueleza
changamoto zinazo wakabili na zilipatiwa majibu kutokana na maswali
waliyokuwa nayo.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments