KUHUSU UCHANGIAJI DAMU SALAMA WIKI HII MKOANI KATAVI,SERIKALI YA MKOA YATUPIWA LAWAMA KUTOUNGA MKOANO ZOEZI HILO
Juni 14 wiki hii ilikuwa ni kilele
cha Siku ya uchangiaji damu salama kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji huduma
ya kuongezewa damu.
Miongoni mwa wahitaji wakubwa wa damu
ni pamoja na mama wajawazito ,watoto wenye umri chini ya miaka 5 pamoja na wagonjwa mbali mbali wenye
uhitaji wa huduma hiyo.
Kupitia kampeni hiyo ambayo ilianza
Juni 1-14,2016,wananchi mkoani Katavi wemetakiwa kuchangia damu salama ili
kuokoa maisha ya wagonjwa.
Hadija Juma Mtalaamu msaidizi wa wa
damu salama Mkoani Katavi akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa
mwitikio wa watu ulikuwa mdogo ambapo hakuna kiongozi yeyote ambaye alijitokeza
kuunga mkono juhudi za uchangiaji damu salama.
Hata hivyo licha ya kuwa kulikuwa na
mwitikio mdogo katika kilelele cha siku ya uchangiaji damu salama katika
viwanja vya shule ya msingi Kashaulili,Hadija alisema kuwa katika maeneo
mengine waliko fika mwitikio wa watu ulikuwa mzuri ukilinganisha huku chanzo cha mwitikio mdogo
ni uhamasishaji hafifu.
Kitaifa kilele cha maadhimisho ya
siku ya uchangiaji damu salama kilifanyika mkoani Dodoma.
Serikali ilikuwa imeweka kiwango cha
chupa zaidi ya 100 kukusanywa kutoka kila mkoa ili kupata damu ya kutosha kwa
ajili ya wagonjwa mbalimbali.
Mwandishi :Issack Gerald Bathromeo
Mhariri : Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments