WAWILI MBARONI AKIWEMO KARANI WA CHUO CHA MAENDELEO MSAGINYA ,KWA SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI KATAVI
Na.Issack
Gerald- Katavi
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linawashikilia
watu wawili akiwemo ASHURA MSAGUSI(30) Karani
wa chuo cha Maendeleo Msaginya Mkazi wa Kata ya Makanyagio na AISHA SUNGURA (28) Mkazi wa mtaa
wa Mji wa Zamani kwa tuhuma za shambulio la mwili.
Kamanda wa Polisi Katavi-Dhahiri Kidavashari |
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo,Kmanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari,alisema kuwa tukio hilo limetokea Mnamo tarehe 17.12.2015 majira ya saa 5 asubuhi katika Mji wa Zamani Kata na Tarafa ya Kashaulili Wilayani Mpanda Mkoani Katavi.
Alimtaja aliyeshambuliwa kuwa ni JENEROZA ROBA(60
Mkazi wa Nsemulwa kwa Mkumbo ambapo alishambuliwa kwa kupingwa ngumi sehemu mbalimbali za mwili wake na
kusababishiwa maumivu makali.
Kamanda Kidavashari alisema kuwa,siku ya
tukio inasemekana kuwa mtuhumiwa ASHURA MSAGUSI alijifanya kupandisha mashetani
na kuanza kumtaja Mtendewa JENEROZA ROBA kuwa anajihusisha na shughuli za
uchawi ambazo zinaathiri familia zao. Kitendo hicho cha kupandisha mashetani kilimshawishi AISHA SUNGURA na hivyo kuungana na ASHURA
MSAGUSI na kuanza kumshambulia mtendewa.
Watuhumiwa wote wawili ambao wanaendelea
kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi na wanatarajia kufikishwa
mahakamani baada ya Upelelezi kukamilika.
Kufuati matukio ya kujichukulia sheria
mkononi,Kamanda wa Polisi anatoa onyo wa watu wenye matukio hayo,ambapo amesema
ataendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa wale watakaoendelea kubainika
kukiuka maagizo hayo kutokana na visingizio mbalimbali.
Endelea kufuatilia habari mbalimbali
kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments