BUNGE NCHINI BURUNDI NA BALAZA LA SENATE NCHINI HUMO WAKUTANA KUJADILI HALI YA USALAMA BURUNDI
Na. Prosper Kwigize
Bujumbura, Burundi
Bunge la Jamhuri ya Burundi kwa pamoja na Baraza la SENATE
leo wamekutana pamoja jijini Bujumbura kujadili hali ya usalama.
Katika kikao hicho kinachoongozwa na spika wa Bunge Bw. Pascal
Nyabenda na Rais wa Senate Reverien Ndikuriyo, wanajadili kuhusu uvumi wa
mauaji ya watusi.
Aidha agenda nyingine ni kujadili kuhusu uharali wa umoja wa
Africa kutuma majeshi nchini humo pamoja na tabia ya washirika ya kimataifa
kuandika ripoti za ongo kuhusu Burundi.
Katika kikao hicho kinachoendelea wabunge na wajumbe wa
Baraza hilo wametaja kuwa uvumi wa mauaji ya kimbali ni wa uongo na kwamba
unalenga kuharalisha hisia za baadhi ya mataifa kutaka kuiondoa serikali
madalakani.
Mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyika kwa kukutanisha
vyombo hivyo viwili unatarajia kutoa tamko la pamoja kulaani mataifa na makundi
ya watu kuichafua Burundi.
Comments