BIL.137 KUGHARIMIA ELIMU BURE JANUARI HADI JUNI 2016
NA:OFISI YA WAZIRI MKUU -DAR ES
SALAAM
SERIKALI
imekwishatenga kiasi cha sh. bilioni 137 kwa ajili ya kugharamia utoaji wa
elimu ya bure kuanzia Januari hadi Juni, mwakani.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa |
Kauli
hiyo imetolewa jana jioni (Jumapili, Desemba 20, 2015) na Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliofika kumsikiliza kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa uwanja wa mikutano wa Likangala
wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.
“Kazi
ya utumbuaji majipu imezaa matunda kwani tumeweza kupata fedha za kugahrimia
elimu ya bure ambayo iliahidiwa na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli wakati
wa kampeni. Fedha hiyo tunayo, na tumeshaanza kuisambaza kwa sababu tunataka
shule zikifunguliwa Januari, 2016 watoto waanze kufaidika,” alisema huku
akishangiliwa.
“Atakayezigusa
fedha hizi na kuzitumia vibaya ni lazima tutamtumbua tu! Tumeshawapa maelekezo
Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Maafisa Elimu wao na kuwaonya kuhusu
matumizi ya fedha hizo,” alisema.
“Hatuhitaji
mwanafunzi achangishwe hela ya mitihani, na zile shilingi 10,000/- kwa ajili ya
wanafunzi wanaosoma Sekondari nazo pia tutazipeleka. Na huu ni mpango wa
dharura ambao haukuwemo katika bajeti ya mwaka 2015/2016, kwa hiyo tutalazimika
kuziombea kibali,” alisema.
Waziri
Mkuu Majaliwa alisema Serikali imekwishafanya hesabu za kubaini kiasi
kinachohitajika kwa ajili ya milo ya watoto shuleni kwa wale walioko bweni na
wale wa kutwa. Hesabu tunazo na tumebaini kuwa tutazimudu,” alisema huku
akishangiliwa.
“Serikali
ilitoa ahadi kwa wananchi na sisi tumedhamiria kuzitekeleza. Tuliahidi elimu
bure nasi tutaitekeleza,” alisema.
Naye
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Bw. Nape Nnauye amewataka
madiwani wa jimbo la Ruangwa kuhakikisha wanamsaidia Waziri Mkuu Majaliwa
kusimamia kazi za jimboni ili aweze kuwa huru kutekeleza majukumu ya kitaifa.
“Madiwani
wa jimbo hili msaidieni Waziri Mkuu kusimamia shughuli za maendeleo ili wakati
yeye anaendelea kutekeleza majukumu ya kitaifa, ya jimbo naye yawe shwari.
Msaidieni kusimamia fedha za umma ziende kwenye miradi iliyokusudiwa ili wakati
akitumbua majipu huko kwingine na huku pia yasiote,” aliongeza.
Endelea kufuatailia
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments