WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUTAMBUA HAKI ZA MTOTO KUZUIA UKATIRI
Na.Agness Mnubi-MPANDA.
WAZAZI
na Walezi mkoani Katavi wametakiwa kutambua umhimu wa haki za watoto na kuepuka
Mazingira yanayopelekea ukatili na unyanyasaji kwa watoto hao.
Akizungumza
na P5 TANZANIA MEDIA na Mpanda Rdaio Mwenyekiti wa Asasi ya Faraja na Urafiki kwa Wanandoa na Ushauri kwa Vijana (FUNUVI
) Bi. Neema Kidima amesema Maelewano mabaya katika ndoa na kutalikia ni miongozni
mwa vyanzo vinavyopelekea kutotambua
haki za watoto na kusabaisha mazingira ya ukatili na unyanayasaji.
Bi.
kidima ameomba Wadau wanaojihusisha na
kupinga ukatili ,Haki za binadamu, pamoja na serikali kushirikiana kutoa elimu
katika jamii juu ya haki za watoto.
Desemba
18 Mwaka huu, watoto 62 wakiwemo
wawili wenye ulemavu wa ngozi (albino) walifichuliwa Wilayani Mpanda na kamati ya baraza la watoto, wakiwa katika mazingira
yanayowanyima haki zao ikiwemo kupatiwa
elimu, kwa kipindi cha mwezi Juni hadi Desemba.
Comments