MGOMO DARADARA MPANDA NAULI KUPUNGUZWA,SUMATRA YASEMA WASIOTAKA NAULI ILIYOPANGWA NA SUMATRA WAPAKI MAGARI
Baadhi ya daradara mjini Mpanda zikiwa zimepaki baada ya madereva kusitisha safari |
Na.Issack Gerald-Katavi
Madereva wa daradara zinazosafirisha
abiria kutoka Mpanda Mjini kuelekea kata ya Kakese leo wamegoma na kumlalamikia
Meneja wa mamlaka ya uasafiri wa majini na nchi kavu Sumatra Mkoani Katavi kwa
kushusha viwango vya nauli.
Madereva hao wakizungumza na Mpanda Radio wamesema
kuwa wamegoma kusafirisha abiria ili kupinga kushushwa kwa viwango vya nauli
ambavyo havikidhi gharama za uendeshaji wa magari yao.
Wamesema kuwa nauli imeshushwa kutoka
shilingi elfu moja na mia tano hadi elfu moja wakati huo wakisema kuwa gharama
ya mafuta basi iendane na kupandishwa kwa viwango vya nauli.
Akizungumza na P5 TANZANIA Meneja wa
Sumatra Mkoa wa Katavi Aman Erasto ili
kujibu shutuma hizo zinazoelekezwa kwake pengine hata katika mamlaka ya usafiri
wa majini na nchi kavu kwa ujumla ameeleza msimamo wa Sumatra kuwa wasiotaka
kutoza kiwango cha nauli ya shilingi elfu moja basi wapaki magari yao au wahame
Mkoa wa Katavi.
Aidha Erasto amesema kuwa watakaotaka
kubadilisha barabara za usafiri kutoka Mpanda kuelekea maeneo mengine tofauti
na Mpanda kwenda Kakese hawatawapatia Leseni watakazozitaka.
Si mara ya kwanza wamiliki wa vyombo
vya usafiri Mkoani Ktavi kugoma kutoa huduma wakitaka masilahi yao kuzingatiwa
na mamlaka zinazohusika na utoaji wa huduma wanayoipata ua kuitoa kwa jamii.
Comments