WATAKAOKAIDI KUONDOKA KATIKA HIFADHI ZA MISITU WILAYANI MPANDA KUONDOLEWA KWA NGUVU
Na.Issack Gerald-Mpanda
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga amepiga
marufu kufanya shughuli za kilimo katika misitu iliyo hifadhiwa akisema kuwa
wanaokaidi na kuendelea kuvamia maeneo ya hifadhi wataondolewa kwa nguvu.
Bi.Matinga ametoa marufuku hiyo leo wakati akieleza za
kuwepo kwa tetesi za baadhi ya wananchi walioondolewa katika maeneo ya hifadhi
kutaka kuendesha shughuli za kilimo.
Aidha amesema
serikali haitakubali kuangamiza uoto wa asili kutokana na watu wanaovamia
misitu kwa kisingizio cha kukosa maeneo ya makazi huku sheria za kupata ardhi
kwa matumizi ya kibinadamu zikiwa wazi.
Miongoni mwa maeneo yaliyokumbuwa na operesheni ya
wananchi kuondolewa kinguvu kwa madai ya kuvamia misitu ni Kijiji cha
Mgolokani kata ya Stalike,Kijiji cha
Nsanda kilichopo kata ya Katumba na maeneo mengine.
Habari zaidi na P5TANZANIA LIMITED
Comments