ZITTO AMEMPONGEZA NYALANDU KUJIUDHURU NDANI YA CCM NA KUACHA UBUNGE
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo),Zitto Kabwe amempongeza
Mbunge wa Singida Kaskazini(CCM), Lazaro Nyalandu kuwa ameonyesha uongozi
uliokomaa.
Zitto ametoa maoni yake hayo baada ya Nyalandu kuamua kujiondoa
CCM na kuachia nafasi yake ya ubunge.
Zitto ameandika, "Lazaro Nyalandu,umeonyesha uongozi. Kwa
namna haki za watu zinavyovunjwa na uchumi wa nchi unavyoporomoka, unahitaji
roho ngumu sana kuwa CCM.Umefanya maamuzi sahihi,wakati sahihi na kwa sababu
sahihi. Kila la kheri."
Lazaro Nyalandu leo ametangaza kujivua nafasi zake ndani ya
Chama Cha Mapinduzi na kuandika barua yake ya kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge
kwa kile alichodai kuwa Chama Cha Mapinduzi na Bunge vimekuwa vikishindwa
kuisimamia serikali na badala yake kutumiwa na serikali jambo ambalo yeye
anaona halina afya katika maendeleo ya nchi na linadidimiza haki
mbalimbali.
Comments