WATU WENYE ULEMAVU MKOANI KATAVI WARIDHISHWA NA HATUA ZA SERIKALI KATIKA KUWAKWAMUA NA UMASKINI
Na.Issack Gerald-Katavi
WATU wenye ulemavu Manispaa ya Mpanda
Mkoani Katavi wamesema wameridhika na hatua zinazochukuliwa na Manispaa ya
Mpanda katika kushughulikia mahitaji yao ikiwemo suala la mikopo.
Hayo yamebainishwa leo katika mkutano
wa hadhara uliofanyika katika shule ya msingi Azimio ukihusisha watu wenye
ulemavu na wataalamu wa idara ya maendeleo ya mjamii Manispaa ya Mpanda kuhusu
masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kupata mikopo na uundaji vikundi vya
kijasiliamali.
Afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya
Mpanda Linus Kalindo pamoja na mambo mengine amewataka watu wenye ulemavu
kutoona ulemavu ni mwisho wa maisha na badala yake waendelee kufuata nmna
wanayoelekezwa ili wapatiwe mikopo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho
la vyama vya watu wenye Ulemavu SHIVYAWATA Mkoani Katavi Issack Mlela amesema watazingatia
yote wanayoshauriwa na wataalamu ikiwemo kuunda vikundi,kusajili vikundi na
hatimaye kupatiwa mikopo.
Hii ni mara ya pili katika kipindi
cha mwezi huu wa Oktoba kwa idara ya maendeleo ya jamii kukutana na makundi
haya ya watu wenye ulemavu ili kusikiliza mahitaji yao na kuwaelekeza namna
wanavyoweza kufanya ili kupata mikopo ya kujikwamua kiuchumi.
Sheria namba 9 ya mwaka 2010
ilipitishwa na bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2010 kwa ajili ya
kusimamia haki za watu wenye ulemavu hapa nchini katika masuala ya afya,elimu
na haki nyingine za kibinadamu
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au
ukurasa P5Tanzania Limited
Comments