WAZIRI WA ELIMU AMETOA AGIZO KALI KWA WAKUU WA VYUO ELIMU YA JUU
Na.Issack Gerald
Serikali
imewaagiza wakuu wote wa vyuo vya elimu ya juu kuacha urasimu katika utoaji wa
fedha kwa wanufaika wa mikopo ambao wana makubaliano na Serikali.
Waziri
wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema leo bungeni
ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Spika Job Ndugai lililotaka
serikali kutoa kauli kuhusu wanafunzi wa mwaka wa kwanza kutakiwa kutoa fedha
ili wasajiliwe kabla ya kupata mikopo.
Agizo
la Spika lilitokana na Mwongozo uliombwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Martha
Mlata ambaye alieleza bunge kuwa wanafunzi wamekuwa wakihangaika vyuoni baada
ya kutakiwa walipe fedha za usajili kabla ya kupewa mkopo.
Amesema
inasikitisha sana kuona baadhi ya vyuo vinadiriki hata kuwakataa wanafunzi
waliowadahili wao wenyewe au vinawalazimisha wachukue programu tofauti na
walizokuwa wamechaguliwa awali na vyuo husika.
Amesema
Serikali haitasita kuchukua hatua kali kwa vyuo vyote vitakavyoleta usumbufu
usio wa lazima kwa wanafunzi na kuwafanya wapoteze muda ambao wanapaswa
kuutumia kwa masomo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments