WAKAZI MKOANI KATAVI WAMETAKIWA KULINDA MIUNDOMBINU YA UMEME
Na.Issack
Gerald-Katavi
Wakazi wa mkoa wa Katavi wametakiwa
kuwa walinzi wa kutunza miundo mbinu ya umeme ili wapate huduma nzuri na
kupunguza kukatika kwa umeme mara kwa mara.
Wito huo umetolewa na meneja wa
shirika la umeme (TANESCO) mkoani katavi mhandisi Julius Sabu ambapo amesema
wananchi wamekuwa wakichangia kuharibika kwa miundombinu hiyo.
Ametaja baadhi ya magari marefu kuwa
miongoni mwa vyanzo vinavyosababisha kukatika nyaya za umeme na hivyo kusababisha hitilafu na hatimaye usumbufu
kwa watumiaji wa nishati hiyo muhimu.
Aidha
amesema shirika la umeme linafanya utaratibu wa kutenganisha laini za makazi ya
watu na maeneo ya viwandani ili kuondosha tatizo la kukatika kwa umeme unaotokana
na matatizo yanayosababishwa na viwanda kutumia laini moja na watumiaji wa
kawaida.
Hata
hivyo amewaomba wananchi kujenga tabia ya kutoa taarifa pale wanapoona kuna
shida ya umeme katika maeneo yao ili kurahisisha kazi na kutatua changamoto kwa
haraka.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments