ZIARA YA SIKU 3 YA MAGUFULI NCHINI UGANDA


Na.Issack Gerald-Katavi

Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli na Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa bomba kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi umefanyika katika kijiji cha Luzinga, jirani na mpaka wa Mutukula.

Pia wamefungua kituo cha forodha chenye huduma zote muhimu kurahisisha safari kati ya nchi hizo mbili.

Ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Hoima -Tanga wenye urefu wa jumla ya Kilometa 1,443 zikiwemo 1,115 zitakazojengwa ndani ya ardhi ya Tanzania utagharimu dola za marekani bilioni 3.55, unatarajiwa kusafirisha mapipa laki 2 ya mafuta kwa siku na unatarajiwa kuzalisha ajira kati ya 6,000 na 10,000.

Taarifa kutoka kurugenzi ya mawasiliano ikulu ya rais nchini inaeleza kuwa rais atakuwa na ziara ya siku tatu nchini humo.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA