VIWANDA 100 VIPYA MKOANI KATAVI LINATEKELEZEKA



Na.Issack Gerald-Katavi

Mratibu wa uwezeshaji wananchi kiuchumi Mkoani Katavi Bw.Torokoko Kayumba amesema agizo la kuwa na viwanda vipya 100 kila mkoa katika kipindi cha mwaka mmoja linatekelezeka.

Bw.Kayumba ametoa kauli hiyo mapema na kusema wameanza kutekeleza agizo hilo na tayari wana viwanda vipya viwili ambavyo vipo katika hatua ya awali.

Amefafanua kuwa kwa sasa serikali Mkoani Katavi  imetenga maeneo katika kila halmashauri kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda huku akiwaomba wananchi kujitokeza katika kuanzisha viwanda.

Kwa mujibu wa Bw. Torokoko Mkoa wa katavi Kwa sasa una jumla ya viwanda vidogo  329,viwanda vya Kati 3 huku viwanda vikubwa kukiwa hakuna hata kimoja.

Kauli hiyo inakuja ikiwa leo ni siku ya uzinduzi kitaifa wa agizo hilo unaofanyika mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na mgeni rasimi ambaye ni waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) Suleimani Jafo.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA