ZIMAMOTO NA UOKOAJI-TAFUTENI VIBALI KABL YA KUJENGA
Na.Issack Gerald-Katavi
Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Katavi limetoa wito kwa wananchi kupata vibali vya ujenzi wa nyumba zao ili kupunguza ujenzi holela.
Hayo yamebainishwa na kamishina msaidizi jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa katavi Kuhindi ambapo amesema majanga mengi yanatokea kwa kutofuata taratibu za namna bora ya ujenzi wa makazi.
Amesema wananchi wanaojenga bila kufuata taratibu na kupata kibali wanasababisha ugumu wa uokoaji katika maeneo hayo pindi majanga mbalimbali yanapotokea.
Hata hivyo amesema kupungua kwa gharama kutoka kiasi cha shilingi 150,000 hadi Shilingi 50,000 kumetokana na tathimini ya muda mrefu ambayo ililenga kuondoa vikwazo kwa kundi kubwa la wananchi ambao wasingeweza kumuda gharama hizo.
Habari
zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments