MKOANI KATAVI AHUKUMIWA JELA MIAKA 20 BAADA YA KUKAMATWA NA NYAMA YA KIBOKO KILO 110
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda imemuhukumu Omary
Maganga (45) kutumikia jela kifungo cha miaka 20 baada ya kupatikana na hatia
ya kukamatwa na nyama ya kiboko zaidi ya kilo 110.
Hukumu hiyo Imetolewa leo Ijumaa na Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda,Chiganga Tengwa baada ya
kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka
uliokuwa ukiongozwa na mwanasheria wa Serikali, Flaviani
Shio.
Awali,katika
kesi hiyo mwendesha mashitaka huyo alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa
Maganga alitenda kosa hilo Oktoba 10 mwaka 2016 nyakati za saa 10 jioni.
Alidai
kuwa siku ya tukio mshitakiwa alikamatwa akiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya
Katavi huku akiwa na nyama ya kiboko yenye uzito wa kilo 118 ambayo thamani
yake Sh 3.2 milioni.
Mwanasheria
huyo wa Serikali ameiambia mahakama kuwa mshitakiwa huyo alikamatwa na askari
wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi baada ya kuwa wamepata taarifa kutoka kwa raia
wema za kuwa mshitakiwa amekuwa akifanya ujangili kwenye hifadhi hiyo.
Akisoma
hukumu hiyo Hakimu Chiganga amesema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani
hapo Mahakama pasipo shaka yoyote inamtia hatiani mshitakiwa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments