MANISPAA YA MPANDA KUADHIMISHA MIAKA 56 UHURU WA TANZANIA BARA KWA KUFANYA USAFI.
Na.Issack Gerald
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi
inatarajia kuadhimisha miaka 56 ya uhuru wa Tanzania bara kwa kufanya usafi
katika maeneo mbalimbali ya Manispaa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu ametaja miongoni mwa maeneo yatakayofanyiwa usafi kwa kushirikisha watumishi wa umma ni pamoja na maeneo ya stendi,Hospitali na maeneo ya soko.

Aidha Nzyungu amewataka wananchi wote kushiriki ipasavyo katika kaufanya usafi katika
maeneo yao ili kuweka mazingira katika hali ya usafi.
Kwa mjibu
wa Bw.Nzyungu zoezi la usafi la kesho katika maeneo yote ya Mkoa wa Katavi
linaratibiwa na uongozi wa Mkoa wa Katavi.
Hatua ya
kufanya usafi siku ya kesho ni utekelezaji wa agizo la rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh.Dkt John Magufuli ambaye miaka miwili iliyopita
aliagiza siku ya jumamosi itumike kwa ajili ya usafi nchi nzima.
Tanganyika(Tanzania bara) ilipata uhuru kutoka kwa Uingereza Demba 9 mwaka 1961 chini ya Rais wa Kwanza wa Tanganyika na Tanzania Julius Kambarage Nyerere ambapo kitaifa maadhimisho yanatarajia kufanyika kesho Mkoani Dodoma maadhimisho ambayo hufanyika Desemba 9 ya kila mwaka.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments