UHABA WA WATUMISHI VITUO VYA AFYA UVINZA NA NGURUKA MKOANI KIGOMA.
VITUO vya afya Uvinza na Nguruka vilivyopo
wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma vinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya
upungufu wa watumishi katika kada zote na hivyo kuathiri ufanisi wakazi ambao
unaweza kusababisha vifo kwa wagonjwa wanaohitaji huduma katika vituo hivyo.
Zena Shaban na Mapinduzi Hamisi ni baadhi ya
wananchi katika wilaya ya uvinza ambapo wameiamba mpanda redio kero wanazo
kumbana nazo namapendekezo yao kwa serikali.
Stanford
Chamgeni ambaye ni mganga mfawidhi wa kituo cha afya Nguruka amesema
wanakumbana na kazi kubwa wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa ambapo kwa siku
hutoa huduma kwa wagonjwa 80 hadi 100 huku mganga wa Kituo cha afya Uvinza
Albert Msingwa akielezea upungufu wa majengo katika kituo chake.
Naye
Mganga mkuu wa Wilaya hiyo Albert Mumwi amekiri mapungufu hayo na kuelezea kuwa
kufikikia sasa tayari wauguzi 10 wamepatiwa ajila na tayari wamepangiwa vituo
vya kazi.
Tatizo
hilo la upungufu wa watumishi limetajwa kuwa kero ya muda mrefu katika vituo
vya afya wilayani uvinza huku idadi ya wakazi ikikadiriwa kuwa 178,189 huku
waganga katika wilaya hiyo wakiwa saba na vituo vya kutolea huduma vikiwa 5.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments