JESHI LA POLISI MKOANI PWANI BADO HALINA TAARIFA ZA KUWEZESHA KUPATIKANA MWANDISHI WA HABARI ALIYEPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA
Na.Issack Gerald
Jeshi la Polisi Mkoani Pwani limesema mpaka
sasa halina taarifa za kutosha zinazowezesha kupatikana mwandishi wa gazeti la
mwananchi Azori Gwanda aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha siku 18
zilizopita.
Kauli hiyo imetolewa na kamanda wa Jeshi hilo
Mkoani Pwani Kashmishna Msaidizi Jonathani Shana ambapo amewataka wananchi wenye taarifa muhimu kuhusu tukio hilo walitaarifu jeshi la polisi ili
lizifanyie kazi.
Katika
hatua nyingine,Kamanda Shana amesema siyo miili yote ilioonekana ikielezea
katika habari ya hindi miezi michache iliyopita inahusishwa na utekaji bali pia
imebainika hata matukio ya ajali,upepo na uzembe wa baadhi ya wahanga
vinahusika.
Mkoa wa
Pwani ni Mkoa ambao umekubwa na matukio watu kupigwa risasi na kuuwawa na watu
wasiojulikana wakiwemo viongozi wa serikali za mitaa na maafisa wa polisi hali
ambayo imesababishwa kuanzishwa mkoa wa kipolisi Mkoani Pwani kama njia
mojawapo ya kudhibiti matukio hayo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments