SOKO KUU LA VYAKULA WILAYANI MLELE KUONDOLEWA KATIKATI YA MJI
Soko kuu la vyakula lililopo katikati ya mji wa
Inyonga katika halmashauri ya wilaya ya mlele mkoa wa katavi linatarajiwa
kuhamishiwa katika eneo la kalovya lililopo katika halimashauri hiyo.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Mlele
Rachel Kasanda wakati akizungumza na wafanya biashara wa wilaya hiyo kwenye
mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari Inyonga.
Katika kikao hicho mkuu huyo wa wilaya pamoja na mkurugenzi mtendaji wa halimashauri hiyo
Alexius Kagunze kwa pamoja wamechangia mifuko kumi ya simenti kila mmoja.
Wakati huo
huo wafanya biashara wa soko hilo wakiuunga mkono jitihada hizo kwa kuahidi
kutoa michango mbali mbali.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments