MKOA WA RUKWA UMESHAULIWA KUONGEZA VITUO VYA HUDMA ZA AFYA
MKOA wa Rukwa umeshauriwa Kuongeza vituo vya kutolea huduma
za afya ili kupunguza mlundikano wa wagonjwa unaoendelea kuongezeka siku hadi
siku kutokana na ongezeko la watu.
Naibu
waziri wa ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Josephat Kandege
alitoa ushauri huo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na uongozi wa mkoa huo
wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi.
Alisema
kuwa hivi sasa mkoa huo unaidadi kubwa ya watu hali iliyosababisha kuwepo idadi
kubwa ya wagonjwa katika maeneo ya kutolea huduma za afya hivyo nilazima
mkakati wakujenga zahanati, vituo vya afya na hospitali uanze mara moja
ilikuendana na idadi ya wakazi wa mkoa huo.
Waziri
Kandege alisema kuwa fursa nyingine iliyopo ni kuyatumia majengo yanayo achwa
na makampuni ya kigeni ya ujenzi wa barabara mkoani humo kwani yakibadilishwa
na kuboreshwa yanaweza kufaa kutumika kutolea huduma za afya.
Alisema
kuwa zipo baadhi ya wilaya hazina hospitali ni vizuri sasa zikajipanga kujenga
ili kuwafikishia wananchi huduma karibu tofauti na hivi sasa wanazifuata mbali
na kuwasababishia gharama na usumbufu mkubwa.
Kwa
upande wake Katibu tawala msaidizi wa mkoa huo Albinus Mgonya anayeshughulika
na tawala za mikoa na serikali za mitaa alimwambia waziri huyo kuwa
uongozi wa mkoa unamipango mingi ya maendeleo lakini changamoto kubwa iliyopo
ni mapato kidogo.
Alisema
kuwa halmashauri za mkoa huo zina kabiliwa na tatizo la mapato kidogo licha ya
kuwa jitihada za kukusanya mapato zinafanyika ikiwemo ni pamoja na kubuni
vyanzo vipya vya mapato sambamba na kutumia mashine za EFDs.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments