DC MPANDA ATAKA JAMII KUACHANA NA MILA KANDAMIZI KWA WANAWAKE NA WATOTO
Na.Issack Gerald
Mkuu wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi
Bi.Lilian Charles Matinga ameitaka Jamii kuachana na mila kandamizi dhidi ya
wanawake na watoto wa kike.
Bi.Matinga ametoa kauli hiyo katika kilele cha
siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya mtoto wa kike na
mwanamke.
Baadhi ya wanawake katika kilele hicho wameelezea mimba za utotoni kuwa changamoto katika maendeleo kwa vizazi vijavyo.
Baadhi ya wanawake katika kilele hicho wameelezea mimba za utotoni kuwa changamoto katika maendeleo kwa vizazi vijavyo.
Aidha
wametaja nafasi ndogo ya ushiriki wa wanawake katika maamuzi ndani ya familia
husababisha kuendelea kwa dhuruma dhidi ya makundi ya wanawake.
Maadhimisho
hayo yamefanyika katika kijiji cha ivungwe,kata ya katumba halamsahuri ya
nsimbo yakiwa na kauli isemyo Funguka ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na
watoto haumuachi mtu salama chukua hatua.
Katika kipindi cha Mwezi Januari mpaka Juni mwaka 2017 jumla ya wanafunzi 14 wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo waliripotiwa kupata ujauzito hali ambayo ilichukuliwa kama ukatiri wa kijinsia.
Katika kipindi cha Mwezi Januari mpaka Juni mwaka 2017 jumla ya wanafunzi 14 wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo waliripotiwa kupata ujauzito hali ambayo ilichukuliwa kama ukatiri wa kijinsia.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments