VIBAKA WATISHIA USALAMA KWA WAKAZI WILAYANI MPANDA MKOANI KATAVI
Na.Issack Gerald
Baadhi ya Wananchi kata ya Misukumilo Manispaa
ya Mpanda wamedai kuingiwa na hofu kufuatia kukithiri kwa matukio ya kiharifu
katika eneo la linalofahamika kwa jina la Migazini.
Wakazi hao wamesema vitendo vya kiharifu katika
eneo la migazini vimekithiri na hivyo kuliomba jeshi la polisi kushughulikia
tatizo hilo.
Wametaja uporaji wa mali za nyumbani na kukabwa
njiani kasha kunyang’anywa mali ni miongoni mwa matukio
yanayofanywa na vibaka hao.
Afisa
mtendaji wa kata hiyo Pasca Mbete amekili kuwepo kwa vitendo hivyo na kuahidi
kuimarisha ulinzi na usalama ili kuondoa adha hiyo.
Kwa upande
wa Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Katavi Damasi Nyanda amewataka wananchi
kutoa ushirikiano ili kuwabaini waharifu hao.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments