WILAYA YA MPANDA IMETENGA HEKA ZAIDI YA 7000 KWA AJILI YA WALIOONDOLEWA KATIKA MAENEO YA HIFADHI
Na.Issack Gerald
Mkuu wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Lilian
Matinga amesema zaidi ya heka elfu saba zimetengwa kwa ajili ya wananchi
walioondolewa katika maeneo ya hifadhi za misitu.
Bi.Matinga amesema kitendo cha uvamizi wa misitu ni uhalifu na kwamba kila mwananchi anapaswa kuishi mahali popote kwa kufuata sheria.
Bi.Matinga amesema kitendo cha uvamizi wa misitu ni uhalifu na kwamba kila mwananchi anapaswa kuishi mahali popote kwa kufuata sheria.
Katika hatua nyingine amewaonya baadhi ya
viongozi wanao warubuni wananchi ili kuyarudia maeneo hayo kuacha maramoja na kuwatadharisha
kuwa sheria itachukua mkondo wake.
Awali
baadhi ya viongozi wa kata ya Stalike ambayo vitongoji vyake vimekumbwa na
sakata hilo wamekana kuwepo kwa maeneo yaliyotengwa kwaajili ya wananchi hao
ambao wanaishi porini.
Sanjari na
hayo viongozi hao wameshutumiwa na wananchi kwa kitendo cha kuwachangisha fedha
kwa madai ya kutaka kuonana na waziri Mkuu ili kulipatia ufumbuzi suala hilo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments